Update:

DC MURO AOKOA JAAZI LA NDOTO ZA WASOMI WA KESHO KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro leo ameungana na wananchi wa kijiji cha LOSIKITO kata ya Mwandeti Halmashauri ya Arusha katika ujenzi wa shule Mpya ya sekondari ya Losiko ambayo inajengwa Kwa nguvu za wananchi.
Dc Muro ameamua kuungana na wananchi katika kuhakikisha shule hiyo inaanza kutumika Mwaka 2019 Kwa lengo la kupunguza uhaba wa shule na vyumba vya madarasa Kutokana na ongezeko Kubwa la wananchi waliofaulu Elimu ya Msingi ambao wanapaswa kuingia Kidato Cha kwanza Mwaka 2019.
Dc Muro anaendelea na ziara yake iliyoanza Leo katika kata ya Mwandeti iliyo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambapo Mkuu huyo wa Wilaya anatarajiwa kutembelea Kata zote 53 za Wilaya ya Arumeru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akifanya ukaguzi kwa moja ya vyumba vya darasa ujenzi wa shule Mpya ya sekondari ya Losiko ambayo inajengwa Kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha LOSIKITO kata ya Mwandeti mkoani Arusha.
Pamoja na kutilia mkazo suala la ujenzi wa maabara zenye vifaa vya kutosha kwaajili ya kuzalisha vijana wenye ujuzi na uelewa wa kisayansi, pia Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro, amesisitiza suala la miundombinu ya viwanja kwaajili ya kuendeleza sekta ya michezo ambayo vipaji vyake huzalishwa toka ngazi za chini, na hapa akitia msumari kuhusu hilo kwa msemo ‘Michezo ni Ajira’.
Ufafanuzi toka kwa kamati ya ujenzi, maswali na majibu ya papo kwa hapo mbele ya Mhe. mkuu wa Wilaya ya Arumeru.