Update:

Walimu Wanaotuhumiwa Kumuua Mwanafunzi Kwa Viboko Wafikishwa Mahakamani

Walimu wawili wa Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba wamefikishwa Mahakamani leo asubuhi Septemba 3, 2018 wakikabiliwea na kesi ya mauaji ya Mwanafunzi Sperius Eradius (13) wa darasa la 5.


Walimu hao waliofikishwa mahakama ya wilaya ya Bukoba kusomewa mashtaka yanayowakabili ni Mwalimu Respicious aliyetoa adhabu ya vibobo na Mwalimu aliyedai kupotelewa na mkoba Elieth Gerald.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 17, 2018 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.