Update:

Mchezaji bora wa FIFA: Ronaldo, Modric na Salah wafika fainali

Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Mohamed Salah ndio wachezaji watatu wa mwisho ambao watawania tuzo la mchezaji bora wa FIFA mwaka huu.
Hakuna mchezaji yeyote aliyekuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe la dunia.
Jopo la wataalamu wa FIFA waliunda orodha ya wachezaji 10 kwa kila tuzo huku manahodha wa timu za taifa, waandishi wa habari na mashabiki wakimchagua mshindi kila kundi likiwa na asilimia 25 ya kura.
Washindi watatangazwa tarehe 24 Septemba huko Royal Festivan mjini London.