Update:

DC MURO ATOA SHUKRANI KWA WANANCHI WA ARUMERU KWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI MBIO ZA MWENGE
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Mh. Jerry Muro  amewashukuru wananchi wote wa Wilaya ya Arumeru kwa kujitokeza kwa wingi wakati wa ziara ya Mbio za Mwenge Kitaifa 2018 ambapo Wilaya ya Arumeru ilipokea Mwenge Kuanzia Tarehe 16/09/2018 na Kuukabidhi Kwa Wilaya ya ARUSHA Mjini Siku ya Jumanne tarehe 18/09/2018 .


Dc Muro Amewashukuru Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Arumeru pamoja na kuwashukuru Wakurugenzi, Watumishi wa Halmashauri Mbili Za Arusha Dc na Meru Dc ambazo ziko Wilaya ya Arumeru pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Vyama Rafiki vya Siasa ambavyo Vilijitokeza na Kuunga Mkono mbio ZA Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao umezindua na Kuweka Mawe ya Msingi ya Miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 19 Kwa Mwaka 2018.


 Dc Muro  Mara ya Baada ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru Kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha *Mhe Gabriel Daqarro* Amewashukuru Sana Viongozi wa Mbio Za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambapo amesema Mbio ZA Mwenge wa Uhuru Kwa 2018 Zimekuwa tofauti kuliko miaka Mingine Kutokana na Umakini,Umahiri na Uweledi wa Wakimbiza Mwenge Wakiongozwa na Ndugu Charles Francis Kabeho  ambao wamesaidia katika Kurudisha Heshima na thamani ya Mwenge wa Uhuru Kwa Kukagua na kutoa Maelekezo ambayo yamesaidia kuongeza  umakini  katika kusimamia Miradi ya Maendeleo pamoja na Fedha zinazotoka Serikali.

*ArumeruYetu* MwengeWetu  *WakatiWetu*

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Arusha Tanzania 

No comments