Update:

Usain Bolt kuanza majaribio ya soka keshoNyota wa mchezo wa riadha aliyeamua kuhamia katika soka Usain Bolt amekiri kuwa na hofu kuelekea mchezo wake wa kwanza wa majaribio akiwa na timu ya Central Coast Mariners inayocheza ligi kuu nchini Australia.

Mshindi huyo mara nane wa medali ya dhahabu ya Olympic katika mchezo wa riadha, anaendelea kujifua kwa nguvu zote akiwa na Mariners na Agosti 31 atashuka dimbani kutupa karata yake ya kwanza kusaka tiketi ya kucheza soka la kulipwa.