Update:

Sababu ya Emmanuel Amunike kuwatema kikosini mastaa wa SimbaWachezaji 6 wa klabu ya Simba wameenguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachojiandaa kwa mechi dhidi ya timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes) Septemba 8 mjini Kampala kwa utovu wa nidhamu.

Kocha wa taifa stars, Emmanuel Amunike amechukua hatua hiyo baada ya wachezaji hao kushindwa kuripoti kambini bila ya taarifa yeyote. Naye katibu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau ameeleza kuwa mbali ya wachezaji hao, viongozi wa klabu hiyo nao watapelekwa katika kamati ya maadili Jumamosi kwa hatua zaidi.