Update:

Majuto kuzikwa leo mkoani Tanga baada ya kuagwa Jijini Dar es Salam


Msanii mwenye heshimu ya hadhi ya juu nchini Amri Athumani maarufu kama ‘Mzee Majuto’ ama KING MAJUTO Unatarajiwa kuzikwa  leo mkoani Tanga.
Mzee King Majuto alifariki dunia  majira ya saa Mbili usiku Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.
Jana, Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk John Magufuli aliwaongoza watanzania kuuaga mwili wa msanii mkongwe wa filamu nchini Amri Athuman maarufu Mzee Majuto.
Tukio hilo lililojaa simanzi ambalo limehudhuria na umati mkubwa wa watu mbalimbali hasa wasanii na wapenda sanaa limefanyika viwanja vya Karimjee, ambapo viongozi wa kitaifa akiwamo Rais mstaafu Jakaya Kikwete na wameshiriki katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuuaga.
Viongozi wengine waliohudhuria shughuli hizo za kuaga ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Zainab Vullu. Wengine ni pamoja na Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


No comments