Update:

WAZIRI KANGI LUGOLA ATEMBELEA KITUO CHA POLISI MURIET JIJINI ARUSHAWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiangalia pikipiki zilizotolewa na
wadau wa kupinga vita uhalifu kwa Kituo cha Polisi Muriet, kilichopo Kata ya Muriet. Kulia ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi.Waziri Lugola yupo jijini Arusha kwa
ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kushoto), alipotembelea nyumba za askari polisi zinazoonekana
pichani, katika eneo la Kata ya Muriet,jijini Arusha.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha,Ramadhani Ng’anzi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kata ya
Muriet, baada ya kutembelea Kituo cha Polisi na nyumba za askari polisi zilizopo eneo hilo.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo (kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani
Ng’anzi (kushoto) kutembelea Kituo cha Polisi cha Muriet (kinachoonekana pichani) na nyumba
za askari polisi zilizopo katika eneo hilo wakati wa ziara yake jijini Arusha. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments