Update:

TANZIA :Mbunge Maji Marefu Afariki Dunia

Mbunge wa korogwe Vijijini Stephen Ngonyani amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya rufaa ya Muhimbili.
Msemaji wa hospitali ya Muhimbili Amilieni Eligaisha alithibitisha kifo cha mbunge Maji Marefu na kusema kuwa alilazwa  katika hospital hiyo juni 9 mwaka huu baada ya kupokelea akitokea hospital ya Mkoani Dodomau
Juni 20, 2018 Majimarefu alihamishiwa kwa ndege kutoka mkoani Dodoma kwenda MNH kwa matibabu.
Hata hivyo kilichokuwa kikimsumbua mbunge huyo hakikuwekwa wazi.
Juni 6, 2018 mbunge huyo alifiwa na mkewe, Mariam aliyekuwa akipatiwa matibabu MNH.
Bunge la Tanzania limeendelea kupoteza wabunge ambapo kifo cha Profesa Majimarefu kinafanya idadi ya wabunge hao kufikia watano.
Wabunge wengine waliofariki dunia ni Dkt. Elly Macha (Viti Maalumu) na Kasuku Bilago (Buyungu) wote wa Chadema. wengine ni Leonidas Gama (Songea Mjini) na Hafidh Ali Tahir (Dimani) wa CCM.