Update:

Congo DR yatangaza kumalizwa ogonjwa wa EbolaJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza rasmi kwamba maambukizi ya ogonjwa wa Ebola yamekomeshwa kikamilifu nchini humo.

Tangazo hilo limehitimisha wiki kumi za maambukizi ya ugonjwa huko nchini Congo ambayo yameua watu wasiopungua 33.

Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Oly Ilunga alitoa tangazo hilo jana Jumanne baada ya uchunguzi wa siku 42 ambako hakukuripotiwa kesi yoyote ya maambukizi mapya ya ugonjwa huo.

Taarifa hiyo ya waziri Ilunga imesema: Kwa ujumla kesi 54 za maambuzi ya ugonjwa wa Ebola zimerikodiwa nchini Congo DR, watu 33 wamefariki dunia na wengine 22 wameokoka janga hilo.Ebola imeua zaidi ya watu 33 Congo DR

Mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola ulianza tarehe 8 Mei mwaka huu katika mji wa Bikoro kwenye mkoa wa Équateur huko kaskazini magharibi mwa Congo na baadaye maambukizi ya ugonjwa huo yalihamia katika mji wa Mbandaka ambao ndio makao makuu ya mkoa huo.

Itakumbwa kuwa, kuanzia mwishoni mwa mwaka 2013 hadi 2016 ugonjwa huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 11 na 300 katika baadhi ya nchi za magharibi mwa Afrika.

No comments