Update:

TUNDU LISSU AMALIZA OPERESHENI YAKE YA MWISHO SALAMA

Operesheni ya mwisho ya Tundu Lissu imefanyika na kumalizika salama.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alifanyiwa operesheni jana, Juni 4,2018 ya kuunga mguu wa kulia.


Katika Operesheni hiyo iliyofanyika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji, Lissu aliizungumzia akisema itakuchukua takriabani saa 8 hivyo kuwaomba Watanzania kumwombea.


Saa 3 usiku jana Juni 4,2018, Mke wake, Alicia ameiambia Mwananchi kutoka Ubelgiji kuwa operesheni imemalizika salama.


"Namshukuru Mungu kwani operation ya 20 iliyokuwa ya masaa 8 imekwenda vizuri na amezinduka. As always he is stable. Asanteni sana," amesema Alicia

Chanzo-Mwananchi

No comments