Update:

TASAF YALETA AHUWENI KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA NGOZI ARUSHA

Kutokana na Mpango wa kuinua kaya masikini serikali kupitia mradi wa TASAF hapa mkoani Arusha umezindua baadhi ya miradi mbalimbali ikiwemo mabweni ya watoto wenye ulemavu wa ngozi vivukio vya waenda kwa miguu ambavyo ndivyo vilivyokua changamoto kubwa kwa wananchi wakata ya Suye pamoja na Kata Ngarenaro kwalengo la kuleta maendeleo kwa wananchi hao
Juma kihamia ni mkurugenzi wa jiji la Arusha ambae ndie alizindua miradi Hio amesema kua nimuhimu wananchi kushirikiana kulinda miundominu hio kwa kila moja kua mlinzi wa mwenzake ili kuiweka miundombinu hio katika Hali ya usalama
Wakizungumza na Sunrise digital wananchi wakata zote mbili kata ya Suye pamoja na Kata Ngarenalo wameelezea namna walivyofurahishwa na ujenzi huo na kutoa changamoto ambazo zilikua zikiwakabili wananchi hao ikiwemo kuwahisha wagonjwa hospitali pamoja na kuwafanya wanafunzi kufika shuleni kwa wakati
Hatahivyo mkurugenzi huyo alipata nafasi ya kuzindua bweni la wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Ya Arusha iliopo Kata ya Kalolen
NA ALOYCE GODFREY

No comments