Update:

PICHA : BASI LA HAMIDA LAGONGA TRENI NA KUUA WATU 10 KIGOMA


Watu 10 wamefariki papo hapo na wengine 23 kujeruhiwa leo baada ya basi kugonga treni ya mizigo katika mkoa wa Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno amesema, basi hilo lilitupwa mita 100 kutoka kwenye eneo la ajali. Amesema waokoaji wamewatoa watu walionaswa kwenye mabaki ya basi hilo, na kwamba huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka.

Kamanda Otieno amesema, basi hilo lilikuwa likitokea Kigoma mjini kuelekea mkoani Tabora, katikati ya Tanzania, huku treni hiyo ya mizigo ikitokea Dar es Salaam kuelekea Kigoma. Amesema uchunguzi unaendelea ili kujua chanzo cha ajali hiyo.

No comments