Update:

MAMA AMCHOMA KWA MAJI MOTO MTOTO KWA MADAI YA KUKOJOA KITANDANI

Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimezidi kukidhiri maeneo mbalimbali hapa mkoani Arusha hususani katika kitongoji cha menyembele Kata ya sekei mara baada ya mama mmoja kumchoma mtoto aliekua akimlea kwa kutumia maji ya moto kwa kudaiwa kua mtoto huyo alikua anakojoa kitandani Hali iliowashangaza wananchi wengi wakata hio
Akizungumza na Mwandishi wa habari za tovuti wa www.sunriseradio.co.tz mwenyekiti Wa kitongoji hicho ndugu Richard Charles amebainisha kutokea kwa tukio hilo na kuchukua jukumu lakumpeleka hospitali kutokana na kuungua sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo maeneo ya kifua pamoja na tumbo
Pia baadhi ya ndugu wa mtoto huyo wamesema kua mama huyo aliemchoma mtoto alimchukua mtoto huyo kwa lengo la kukaa nae ili kumsaidia shuhuli mbalimbali zanyumbani pamoja na kumpeka shule hali iliogeuka nakutokea kwakitendo hicho
Johnson singoi laiza ni polisi jamii wa Kata hio amesema kua wamekua wakijitahidi kudhibiti vitendo hivyo mara Kwa mara nakutoa wito kwa wananchi pamoja na wazazi kutojichukulia sheria mkononi
Mwanahabari:Aloyce Godfrey

No comments