Update:

Iran yawa nchi ya Kwanza kuwasili kwa ajili ya michuano hiyo

Ukiachilia mbali wenyeji wa michuano hiyo Russia, kati ya timu za mataifa 31 ambazo zinashiriki michuano ya kombe la dunia, Iran imekuwa ya kwanza kuwasili ilipotua jana kwenye uwanja wa Vnukovo mjini Moscow.
Kocha mkuu wa timu hiyo Carlos Queiroz amesema ni fahari kubwa kuwa miongoni mwa timu zinazoshiriki michuano hiyo, hivyo ni sababu pekee inayoweza kuwafanya wafike mapema.
Hii ni mara ya tano kwa Iran kushiriki kombe la dunia kwani waliwahi kufanya hivyo pia mwaka 1978, 1998, 2006 na 2014.
Mwaka huu, Iran iko kundi B pamoja na timu za Hispania, Ureno na Morocco, mechi yao ya kwanza ikiwa ni dhidi ya Morocco Juni 15 mjini St. Petersburg.

No comments