Update:

Shambulio laua watu 45 katika jimbo la Kaduna Nigeria

Taarifa ya polisi ya Nigeria iliyotolewa leo imesema kuwa, mauaji hayo ya kutisha yalitokea siku ya Jumamosi na kwamba, hadi sasa watu waliotekeleza shambulio hilo hawajajulikana.
Inaelezwa kuwa, kijiji cha Gwaska kinachopatikana katika eneo la Birnin-Gwari, kiko karibu na eneo la msitu linalojulikana kwa uhalifu mkubwa.
Ripoti za awali zinasema kuwa, waliotokeza shambulio hilo ni genge la wahalifu kutoka katika jimbo la jirani la Kaduna la Zamfara.
Wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram
Ripoti zaidi zinaeleza kuwa, viwiliwili 45 vimepatikana vikiwa vimetapakaa katika msitu.
Nchi ya Nigeria imeendelea kushuhudia machafuko hasa mashariki mwa nchi hiyo kutokana na kuweko harakati za kundi la kigaidi la Boko Haram.
Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.
Tokea kundi la kigaidi la Boko Haram lianzishe uasi wake nchini Nigeria mwaka 2009, watu zaidi ya 20 elfu wameuawa. Aidha zaidi ya watu milioni mbili wamekuwa wakimbizi kutokana na ugaidi wa Boko Haram. 
Kwa sasa wigo wa harakati na mashambulio ya Boko Haram umepanuka hadi katika nchi jirani za Cameroon, Niger na Chad