Update:

MVUA YASABABISHA KIFO CHA MUUGUZI WA HOSPITALI YA ST.ELIZABETHMvua iliyokuwa ikinyesha Alfajiri ya Leo May 16,Mwaka huu imesababisha kifo cha muuguzi Mmoja Wa kike Wa hospital ya Wilaya ya St Elizabeth ambaye amesombwa na mafuriko wakati akielekea kazinikwake.
Kwa mujibu Wa mganga Mkuu Wa hospital hiyo Dkt Joslin Mlay amemtaja marehemu kuwa ni AlodiaSilvesta anayekadiliwa kuwa na umri Wa miaka 60
Amesema muuguzi huyo amekumbwa na masahibu hayo umbali wa Mita mia moja kabla ya kufika hospitalini hapo majira ya  Asubuhi katika ukuta wa kanisa la Lutheran uliopakana na hospital hiyo ya st Elizabeth.
'Marehemu alikuwa akivuka kidaraja kidogo ndipo alipoteleza na kusomba na maji ya mvua umbali Wa Mita 100 ambapo kikosi cha zima moto na wokozi waliweza kutoa mwili uliokuwa umekwama kwenyeKara Vatican edema Dkt Mlay
Mwili Wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospital ya rufaa ya Mount Meru Mkoa Wa Arusha
Na Joseph Ngilisho