Update:

MSUVA AANZA VIZURI HATUA YA MAKUNDI AFRICA

Winga wa zamani wa Yanga Simon Msuva, ambaye kwasasa anachezea klabu ya soka ya Difaa El-Jadida ya Morocco ameanza vizuri hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Africa baada ya kutoa sare ugenini.

Difaa El-Jadida jana usiku ilicheza mchezo wake wa kwanza katika hatua ya makundi dhidi ya Mouloudia Club D’Alger ya Algeria na kutoa sare ya 1-1 kitu ambacho kinaiweka katika hali nzuri ya kufanya vyema katika michezo ya nyumbani.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Julai 5, 1962 jijini Algiers, Msuva alicheza dakika 87 na kutoa mchango mkubwa katika sare hiyo na sasa watasubiri katika mchezo wao wa nyumbani ili kufanya vizuri.

Msuva ameifungia mabao 5, Difaa El-Jadida katika michuano hii. Timu hiyo imepangwa Kundi B pamoja na timu za Mouloudia Club D’Alger, E. S. Setifienne ya Algeria na TP Mazembe ya DRC.