Update:

Meneja mpya wa Arsenal kujulikana kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia.Klabu ya soka ya Arsenal inauhakika wa kumtangaza meneja mpya wa timu hiyo atakayechukua mikoba ya Arsene Wenger, kabla ya kuanza kwa fainali za michuano ya kombe la dunia.

Washika bunduki hao wa London,hawajaweka hadharani lini itakuwa muda rasmi mwisho wa kusaka meneja mpya, lakini meneja mpya atajulikana kabla ya Mei 14, tarehe ambayo michuano ya kombe la dunia itakuwa inaanza kutimua vumbi huko nchini Urusi.

Wenger aliyedumu katika klabu ya Arsenal kwa miaka 22, ataingoza timu hiyo katika michezo miwili iliyosalia kabla ya kumalizika kwa ligi jumapili ya Mei 13.