Update:

Maparomoko ya ardhi yaua watu 23 Ethiopia, mvua kubwa zaendeleaWatu 23 wamefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katikati ya Ethiopia.

Vyombo vya habari vya huko vimesema maporomoko hayo yametokea katika eneo la Oromia ya Kati baada ya mvua kubwa kunyesha kwa saa kadhaa.

Mvua kubwa zimeanza nchini Ethiopia, wakati msimu wa mvua unawadia. Mvua hizo huwa zinasababisha maporomoko ya udongo katika baadhi ya sehemu.

Hali kama hiyo pia imeripotiwa katika nchi jirani ya Kenya ambapo mvua kubwa zimesababisha maafa makubwa ambapo watu zaidi ya 120 wamepoteza maisha tokea mwezi Aprili.
Mafuruko nchini Kenya

Katika nchi jirani ya Somalia pia kimbunga ambacho kiliandamana na mvua kubwa na upepo mkali kimesababisha watu 47 kupoteza maisha katika eneo la Somaliland. Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yametoa wito kwa wafadhili kuwasaidia walioathirika na kimbunga hicho kilichopewa jina la Sagar ambacho kilikumba pwania ya eneo hilo wiki iliyopita.

No comments