Update:

Kocha wa zamani wa Yanga afariki duniaKocha wa zamani wa Yanga, Jack Chamangwana amefariki dunia jana jioni baada ya kuumwa ghafla na kulazwa, lakini juhudi za madaktari hazikufanikiwa kuokoa uhai wa nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi.

Chamangwana alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Malkia Elizabeth jijini Blantyre na amefariki akiwa na umri wa miaka 61. Imeripotiwa kuwa kocha huyo alikuwa akisumbuliwa na Shinikizo la damu.

Aidha, Mtalaam huyo wa ufundi aliyeifundisha Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000, alikuwa akifanya kazi na klabu ya Be Forward Wonderers inayoshiriki ligi kuu ya Malawi kama Mkurugenzi wa Ufundi.

Hata hivyo, Jack aliichezea timu ya taifa ya Malawi kwa mara ya kwanza mwaka 1975 akiwa na umri wa miaka 18, kwenye mechi dhidi ya Kenya jijini Lilongwe. Pia aliiongoza Malawi kutwaa ubingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) mwaka 1978/79