Update:

Gor Mahia, Rayon Sport na Yanga, kuiwakilisha Afrika Mashariki leo

Leo zinapigwa mechi za raundi ya pili ya kombe la Shrikisho la soka barani Afrika kwa ngazi ya klabu ambapo timu tatu za Afrika mashariki zitalamika kucheza ili kurekebisha makosa ya kimatokeo kwenye mechi zake za kwanza.
Young Africans ya Tanzania ambayo katika mechi yake ya kwanza ilifungwa kwa magoli 4-0 na USM Algiers ya Algeria, leo itawakaribisha wanaAfrika mashariki wenzao Rayon Sport kutoka Rwanda ambao wenyewe kwenye mechi yao ya kwanza walipata sare ya magoli 1-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Lakini Kibarua kingine kitakuwa ni kwa Gor Mahia ambao watakuwa nyumbani mjini Nairobi kuwakaribisha USM Algiers.