Update:

Wapinzani wa Madrid hakuna mbabe, Arsenal yashinda dhidi yaArsenal jana imepata ushindi wa magoli 3-2 kwenye mechi yake ya 32 ya ligi kuu nchini Uingereza ilipocheza dhidi ya Southampton wake wa nyumbani wa Emirates.

Magoli ya Arsenal yalifungwa na Danny Welbeck aliyefunga mawili na moja likifungwa na Pierre Emerick Aubameyang ambapo magoli ya Southampton yakifungwa na Charlie Austin na Shane Long.

Kwingineko nchini Hispania mchezo wa wapinzani wa mji mmoja wa Madrid (Atletico na Real) walichoshana nguvu baada ya mechi yao kuisha kwa sare ya magoli 1-1.

Goli la Real Madrid lilifungwa na Cristiano Ronaldo likiwa la kutangulia lakini Antoinne Grizmanne akisawazisha katika dakika nne baadaye.

No comments