Update:

Waandamanaji CAR waweka maiti mbele ofisi ya Umoja wa Mataifa BanguiMamia ya waandamanaji waliokuwa na hasira leo Jumatano wameweka maiti za watu wasiopungua tisa waliuawa katika mapigano katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mbele ya makao makuu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa, mjini Bangui.


Maandamano hayo ya kuweka maiti katika ofisi za Umoja wa Mataifa yamesadifiana na safari ya mkuu wa timu ya umoja huo inayosimamia amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jean-Pierre Lacroix.

Waandamanaji hao wanawalaumu askri wa kimataifa kwamba wameshindwa kukomesha ghasia na mauaji nchini humo hususan katika mji mkuu, Bangui.

Wakati huo huo kikosi cha askari Umoja wa Mataifa wanaolinda usalama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA kimetangaza kuwa askari mmoja wa UN kutoka Rwanda ameuawa na wengine 8 wamejeruhiwa katika mapigano yaliyojiri baina ya wanajeshi hao na makundi ya waasi katika wilaya yenye idadi kubwa ya Waislamu ya PK5 mjini Bangui.

Waasi wa Anti Balaka

Eneo hilo limekuwa likilengwa mara kwa mara kwa mashambulizi ya kundi la waasi wa Kikristo la Anti-balaka.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limeripoti kuwa imetoa matibabu kwa zaidi ya watu 40 waliojeruhiwa katika machafuko hayo.

No comments