Update:

Vyama vya Riadha vya Tanzania, Afrika na Dunia vyaafikiana kuhusu mshiriki wa timu ya Tanzania Anthony Tapson MwangaSakata la mwanariadha wa mbio za kuruka vihunzi wa timu ya Tanzania inayotarajia kushiriki mashindano ya Jumuiya ya madola nchini Australia Anthony Tapson limetatuliwa baada ya nyaraka zenye maelezo yake ya binafsi kuwasili.

Anthony aliwekewa pingamizi na shirikisho la riadha la kimataifa IAAF, baada ya kutomtambua kama Mtanzania bali Muafrika kusini jambo ambalo kwa mujibu wa nyaraka hizo, yeye ni mtanzania anayesoma Afrika Kusini lakini amekuwa akishiriki mingi ya michezo ya IAAF akiwa Afrika Kusini.

Chama cha riadha cha Tanzania kimewasilisha nyakala za Anthony pamoja na za baba yake mzee Tapson Mwanga ambaye ni mwenyeji wa Kilimanjaro Tanzania.

Kwenye mashindano hayo yanayoanza rasmi kesho April 4, Tanzania inawakilishwa na wanamichezo 19.