Update:

Vieria kumrithi Wenger ArsenalNguli wa zamani wa Aresenal, Patrick Vieira anatarajiwa kuerejea katika kikoci cha timu ya Arsenal akiwa kocha.

Nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo na Ufaransa, anahusishwa na mpango wa kutua Emirates kujaza nafasi ya Arsene Wenger.

Wenger anatarajiwa kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu, baada ya kushindwa kuipa labu hiyo mafanikio kwa muda mrefu.

Habari zanaeleza kuwa, Wenger atabaki katika klabu hiyo akiwa ni mmoja wa vigogo watakaokuwa katika benchi la ufundi.