Update:

UEFA yalaani vikali vitisho vinavyotolewa dhidi ya refarii Michael OliverShirikisho la vyama vya mpira wa miguu vya barani Ulaya, limelaani vikali vitisho na matusi vinavyoelekezwa kwa mwamuzi wa ligi kuu nchini Uingereza Michael Oliver na mkewe Lucy.

Vitisho hivyo vinavyotolewa na wafuasi wa timu ya Juventus ya Italia pamoja na baadhi ya mashabiki wa soka wa nchini Italia, vinadaiwa kuja baada ya Michael Oliver kuizawadia Real Madrid penati katika mechi ya robo fainali ya klabu bingwa Ulaya ilipocheza dhidi ya Juventus.

Polisi nchini Uingereza imetangaza kufuatilia kwa makini usalama wa Michael Oliver na Mkewe, na kamati ya waamuzi ya UEFA imetangaza kuwalinda waamuzi wake hao.

Aidha kauli ya kulaumu ya Buffon imepokelewa kwa mitazamo tofauti iliyoitafsiri kuwa siyo ya kiuanamichezo, lakini mwenyewe akijitetea kuwa ilikuwa ni kutokana na mapokeo ya presha ya matokeo.