Update:

Timu ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yashinda ubingwa wa mashindano ya Afrika Mashariki na kati


Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imetwaa ubingwa wa mashindano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U17 Championship) yaliyofanyika nchini Burundi baada ya kuwafunga Somalia kwa magoli 2-0 katika mchezo wa fainali.
Magoli ya Ushindi kwa timu hiyo yalifungwa na Edson Jeremiah dakika ya 25 pamoja na Jaffar Mtoo kunako dakika ya 66.
Na katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu uliofanyika siku ya jumamosi, Uganda walipata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Kenya.
Tanzania ndiyo itakuwa timu mwenyeji wa Mashindano ya vijana ya Afrika mwaka 2019.