Update:

Sweden, FA wamtangaza Zlatan kutocheza kombe la dunia 2018

Baada ya fununu za muda mrefu kuwa nyota wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic kuwa atabadili maamuzi yake ya kustaafu na kuichezea timu yake ya taifa ya Sweden katika fainali za kombe la dunia nchini Urusi, kiongozi wa FA ya Sweden, Lars Ritch baada ya kufanya mazungumzo ya kina na mchezaji huyo, ameamua kutoa majibu hadharani kuwa nyota huyo amekataa kubadili maamuzi yake ya kustaafu na kurudi kuichezea timu yake ya taifa katika michuano hiyo.