Update:

Nusu ya Makamishna wa Tume ya uchaguzi Kenya wajiuzuluMgogoro ndani ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya IEBC unaendelea kutokota huku nusu ya makamishna wa tume hiyo wakitangaza kujiuzulu.

Miongoni mwa makamishna waliotangaza kujiuzulu leo Jumatatu ni pamoja na Naibu Mwenyekiti, Connie Nkatha Maina. Makamishna wengine waliotangaza kujiuzulu kutokana na kile walichokitaja kuwa ni kutokuwa na imani na Mwenyekiti Wafula Chebukati ni Margaret Mwachanya na Paul Kurgat.

Akisoma taarifa mbele ya waandishi wa habari jijini Nairobi hii leo kwa niaba ya makamishna wenzake, kamishna Margaret Mwachanya amesema, "Mwenyekiti ameshindwa mara kadhaa kusimama kidete ili kudhibiti jahazi la tume hiyo ambalo limekuwa likiyumba tangu wakati wa uchaguzi wa Agosti 8 mwaka jana."Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alishinda uchaguzi tata wa marudio uliosusiwa na Raila Odinga, Oktoba 26

Amesema ili kurejesha imani ya wananchi kwa IEBC, tume hiyo inapaswa kuzuia uingiliaji wa masuala ya chombo hicho cha kusimamia uchaguzi kutoka kwa asasi na maafisa ajinabi.

Oktoba mwaka jana, Roselyn Akombe, mmoja kati ya makamishna wanane wa IEBC alitangaza kijiuzulu akiwa nje ya nchi, ambapo alisisitiza kuwa amechukua uamuzi huo kutokana kwamba hana imani iwapo IEBC ingeweza kusimamia uchaguzi wa tarehe 26 ya Oktoba mwaka jana au la na kwamba tume hiyo imedhibitiwa na pande ambazo hata hivyo hakuzitaja.Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati