Update:

MZEE WA MIAKA 60 AKUTWA AMEKUFA MAENEO YA SOKO LA SAMUNGE JIJINI ARUSHA

Eneo alilokua amelala marehemu.  


Mtu mmoja anaye kadiriwa kua na umri wa miaka 60-70 amekutwa amekufa katika soko la Samunge lililopo katika Kata ya Kati mkoani Arusha huku chanzo cha kifo hicho kikishindwa kubainika kutokana na mwili wa marehemu huyo kutokua Na majeraha ya aina yeyote

Akizungumza na sunrise Digital Plus shuhuda wa tukio hilo ambaye pia nimfanyabiashara katika soko hilo anayejulikana kwa jina la Jafari amesema kua yeye amemkuta marehemu katika kibanda chake majira ya saa kumi alfajiri pindi alipoenda kufungua biashara yake nakutoa taarifa kwa walinzi wa soko hilo

Pia afisa mtendaji wa kata hio ndugu mgunda mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kua taarifa hizo amezipata saa mbili asubuhi pindi akiwa ofisini kwake na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mkoani hapa kwaajili ya uchunguzi wa mwilihuo

Na. Aloyce Godfrey

No comments