Update:

MBOWE NA VIONGOZI WENGINE CHADEMA WAMETIMIZA MASHARTI YA DHAMANA.....HALIMA MDEE KASOMEWA MASHITAKA MAWILI


Viongozi 6 wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Washtakiwa hao walitakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh20 milioni na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao ama wa vijiji au mtaa, ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee yeye amesomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa.

No comments