Update:

Mama na Mtoto wanusurika kifo kwa kudondokewa na nyumba

Mama na watoto wake wawili  wamenusurika kifo kwa baada ya kudondokewa na nyumba waliyokua  wanaishi katika Kata ya Majengo,  Manispaa ya kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.
Akizungumza na Wandishi wa Habari, moja kati ya Mhanga wa ajali hiyo  Site Hussen  alisema chanzo cha ajali hiyo ni  barabara iliyokua ikitengenezwa mtaani hapo na kusababisha nyumba nyingi mtaani hapo kuwa na nyufa.


“Ilikua Majira saa 7 usiku wa ndipo tulipo ndondokewa na nyumba mimi na watoto wangu wawili nilisikia kama nyumba inatikisika kisha undongo ukadondoka ikabidi niwahi kuangalia watoto wangu nilipofika chumbani ndipo ukuta wa nyumba ukatudondokea," alisema Hussen.


Kwa upande wake Mwanaharusi  Hamisi  Mkazi wa Mtaa wa Majengo alisema nyumba nyingi katika mtaa huo zimepata nyufa kutokana na ujenzi wa  barabara, isitoshe msimu huu ni wamvua bado wana wasi wasi kuendelea kutokea kwa matukio mengine kama haya.


"Tunalalamika kulipwa fidia kwa madhara tuliyo yapata kutokana na ujenzi huu lakini hatujalipwa chochote hata kama ni kidogo tungepewa angalau tukaziba nyufa katika nyumba ili kuzuia madhara kama haya kujitokeza  tena lakini tunaambiwa kuna marekebisho  tulienda mwezi jana lakini tunajiuliza haya marekebisho mpaka lini,” alisema hamisi


Mganga mfawidhi wa  zahanati ya Kigoma Uijji   Ezie Mbwana  amethibitisha kupokea majeruhi  hao ambao ni mama na watoto wawili wote wa familia moja na  kusema   mtoto mmoja alipata majeraha kichwani hivyo  jitihada zinaendelea kuwahudumia majeruhi hao na wanaendelea vizuri kwa sasa.