Update:

Mabeyo aomba mpambe wa Rais apangiwe kazi nyingine

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Venance Mabeyo amemuomba Rais John Magufuli aridhie mpambe wake (Rais), Kanali MN Nkelemi, kupangiwa kazi nyingine. Mabeyo ameyasema hayo leo Aprili 12, wakati alipokuwa akitangaza uteuzi wa Rais wa majenerali na makanali 28 Ikulu jijini Dar es Salaam. “Kanali Nkelemi, yeye kwa sasa ni mpambe wa Rais na kwa cheo hicho namuomba Rais aridhie nimpangie kazi nyingine,” amesema Mabeyo. Pia Mabeyo alitangaza kuwapandisha vyeo makanali 28 kuwa mabrigedia jenerali.
SOURCE:MWANANCHI

No comments