Update:

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) Man City wapigwa butwaa katika dimba la Anfield, Barca yaifumua AS RomaMichuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) hatua ya robo fainali usiku wa kuamkia leo iliendelea tena kwa michezo miwili kupigwa, FC Barcelona wakiwa katika uwanja wao wa Nou Camp walicheza dhidi ya AS Roma wakati Liverpool walicheza na Manchester City katika dimba la Anfield.

Mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Man City ndio ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu usiku huo, hii inatokana na kuzikutanisha timu zinazotoka ligi moja (England) kucheza zenyewe kwa zenyewe, Liverpool wakiwa nyumbani katika uwanja wao wa Anfield wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ya Liverpool yakifungwa na Mohamed Salah dakika ya 11, Chamberlain dakika ya 21 na Sadio Mane dakika ya 31.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya FC Barcelona waliikaribisha AS Roma, Barcelona wameinyuka AS Roma kwa jumla ya magoli 4-1.

No comments