Update:

Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya, Mussa Taibu adhibitisha kutokea kwa ajali mbeyaLeo April 9, 2018 Watu wanane wa familia moja wamefariki papo hapo baada ya gari dogo aina ya Noah waliyokuwa wakisafiria kutoka Chunya kwenda Jijini Mbeya, kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Igembesabo katika eneo la Igodima Mbeya.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mussa Tahib ni kwamba ajali hiyo imetokea saa 5:00 asubuhi nakusema kuwa wanafamilia hao waliofariki walikuwa wanawahi mazishi ya ndugu yao jijini Mbeya.

Amesema wanafamilia hao walikuwa tisa na kwamba ni mmoja pekee ambaye alisalimika japo alijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya kwaajili ya matibabu na hakuna majeruhi wala kifo chochote kwenye basi.

No comments