Update:

India yatuhumiwa kutumia dawa michezoniKocha wa timu ya masumbwi ya India inayotarajiwa kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola nchini Australia Santiago Nieva amekanusha tuhuma za kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizokatazwa michezoni.

Waandaaji wa mashindano hayo wameishitaki timu ya India baada ya kukuta sindano za kitabibu katika vyumba vya mabondia wake.

Katika utetezi wake kocha Santiago amesema sindano hizo ni za chanjo ya vitamin kwa moja ya mabondia ambaye hali yake si nzuri.

Kukutwa na sindano ni kosa kwa mujibu wa sera ya kimataifa ya mashindano isemayo "no needle" yaani zuia matumizi ya sindano.

Kwa kuwa mashindano hayo yanaanza rasmi kesho, kamati ya michuano ya jumuiya ya madola inatarajiwa kutoa majibu ya hatma ya kesi hiyo leo baada ya kukaa na kujadili.