Update:

Chris na Tanisha washinda ubingwa wa Uingereza Mbio za kubebana mgongoni

Chris Hepworth na Tanisha Prince ndiyo mabingwa wa Uingereza kwa mwaka huu katika mbio maalum za kubebana mtu na mke wake baada ya kuwashinda wenzao katika mbio hizo za umbali wa mita 380 zilizofanyika mjini London.
Kutokana na ushindi huo, Chris na Tanisha wamefuzu kwa ajili ya mashindano ya dunia yatakayofanyika nchini Finland mwezi Julai mwaka huu, lakini wakapata za ya pipa lenye bia.
Naye mshindi wa mwisho hupewa zawadi ya kifuta jasho ambayo ni tambi na chakula cha mbwa.
Kutokana na hatari iliyopo kwenye mchezo huo, masharti ni kuwa washiriki lazima wawe na umri usiopungua miaka 18, wawe na uzito usiopungua kilo 50 na zaidi ya hapo adhabu kali hutolewa kwa wale wanaowaangusha wenzi wao.