Update:

Bondia Anthony Joshua aanza mipango ya kujiandaa na pambano dhidi ya Deontay WilderBondia Anthony Joshua aanza mipango ya kujiandaa na pambano dhidi ya Deontay Wilder

Mwanamasumbwi raia wa Uingereza Anthony Joshua AJ amesema yuko tayari na atapokea wito kwa mikono miwili endapo bondia Mmarekani Deontay Wilder atatoa mwito wa kupigana naye.

AJ amesema tena atakuwa tayari kuweka rehani mikanda yake yote minee kwenye pambano hilo kwa kuwa anaamini itakuwa ndiyo kitovu cha heshima ya ubondia wake.

Kwa kuwa mara kwa mara Deontay ameendelea kusisitiza kwa kubeza ushindi anaopata, AJ amesema timu yake inaanza mpango wa kuweka mikakati kwa ajili ya pambano dhidi ya Deontay.

Na kuhusu, suala la mahali pa kufanyia pambano hilo, AJ amesema kwa kuwa yeye ni bingwa wa dunia, na yupo tayari kupigana katika nchi yoyote ama mji wowote.

No comments