Update:

BASI LA CITY BOYS LAGONGANA NA LORI NA KUUA WATU 12,KUJERUHI ZAIDI YA 40 TABORA

Watu 12 wamepoteza maisha na wengine 46 kujeruhiwa baada ya basi la City Boys lililokuwa linatoka Karagwe kwenda Dar es salaam kugongana na lori katika eneo la Makomero wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora.


Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 4,2018.


Inaelezwa kuwa gari lenye namba za usajili T486 ARB Fuso likiwa na mzigo wa viazi likitokea Singida kuelekea Igunga lilipasuka tairi ya kulia na kutumbukia katika mashimo mawili barabarani na kukosa uelekeo na kugonga basi la abiria T983 DCE Scania kampuni ya City Boys.


Chanzo cha habari cha Malunde1 blog kinasema watu 10 walifariki katika eneo la tukiona wawili wakiwa wanapelekwa hospitali ya wilaya ya Igunga.


Aidha majeruhi 46 wamefikishwa katika hospitali ya Igunga kwa matibabu kati yao watatu ni mahututi na wawili wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando na amepelekwa hospitali ya Nkinga.


Dereva wa basi pia alipoteza maisha papo hapo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba atatoa taarifa rasmi baadae.
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Muonekano wa basi la City Boys baada ya ajaliNo comments