Update:

Barcelona yashindwa kutangaza Ubingwa baada ya sare na Celta Vigo

Nchini Hispania Barcelona imeendelea kuvutwa shati katika mbio zake za kutangaza ubingwa baada ya kuambulia pointi moja tu kwenye mchezo wa jana ilipocheza dhidi ya Celta Vigo.


Licha ya kutangulia kufunga magoli ya kuongoza mara mbili, Barcelona ilijikuta ikiwaruhusu Celta kusawazisha na matokeo kuwa mbilimbili.


Barcelona sasa inafikisha pointi 83 na ikiwa imesaliwa na mechi tano za ligi msimu huu.


Katika mechi zingine zilizopigwa jana, Villareal ilishinda kwa magoli 2-0 dhidi ya Leganes na Deportivo la Coruna ilitoka sare ya bilka kufungana na Sevilla


No comments