Update:

Baraza la Usalama lalaani shambulio dhidi ya walinda amani nchini CARBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio dhidi ya askari jeshi wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati lililosababisha mauti ya mwanajeshi mmoja raia wa Rwanda na kujeruhi wengine wanane.

Baraza la Usalama la UN jana lilitoa taarifa likieleza kusikitishwa na mauaji hayo na kutoa mkono wa pole kwa familia ya mwanajeshi huyo aliyeuawa. Baraza hilo limetaka askari jeshi waliojeruhiwa wapatiwe matibabu haraka iwezekanavyo. Baraza la Usalama limebainisha masikitiko yake kufuatia kuuliwa na kujeruhiwa makumi ya raia Jumapili iliyopita huko Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati; na kulaani pia machafuko yaliyoikumba kata moja huko Bangui wakati wa kufanyika zoezi la kuwapokonya silaha na kuwatia mbaroni wanamgambo wenye silaha.
Majeruhi wakipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi na vitendo vyote vyenye kuzusha machafuko dhidi ya askari jeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (MINUSCA) vinavyofanywa na makundi yenye silaha na wahalifu wengineo na kusisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya askari jeshi wa kulinda amani yatasababisha jinai za kivita. Baraza hilo aidha limevikumbusha vyama vyote vya kisiasa kuheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu.

No comments