Update:

Baldev Chager :Bingwa mpya mbio za magari 2018Baldev Chager ndiye bingwa mpya wa mashindano ya magari ya Afrika kanda ya Mashariki yaliyofanyika nchini Kenya.

Baldev alifanikiwa kuongoza tangu mwanzo mpaka mwisho katika hizo zilizodumu kwa siku tano na zikiwa na urefu wa kilomita 1500 katika nyika kuanzia Nanyuki hadi Nakuru.

Akitumia gari aina ya Porsche toleo namba 911, Baldev aliwashinda madereva wengine 37 walioshiriki na kwa upande wa wanawake mshindi alikuwa Lola Verlaque ambaye alikuwa anatumia gari aina VW Golf Gti.

Mshindi wa pili kwa upande wa wanaume alikuwa Geof Bell akitumia gari aina ya Datsun, na mshindi wa tatu alikuwa Onkar Rai kwa kutumia gari aina ya Porsche.

No comments