Update:

Baadhi ya mataifa ya Ulaya yamekataa kuwakamata wahusika wa mauaji ya kimbariRwanda imeyalaumu tena mataifa mbalimbali ya Ulaya kwa kkile ilichosema kuwa, kushindwa kwa mataifa hayo kuwakamata watu waliohusika katika mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Watutsi mwaka 1994.

Lawama hizo zilitolewa Ijumaa ya jana jijini Kigali wakati wa kutamatisha wiki moja ya kumbukumbu ya mauaj hayo mabaya katika historia ya nchi hiyo.

Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Baraza la Seneti Bernard Makuza amesema kuwa, serikali ya Rwanda haitozivumilia nchi hizo.

Miongoni mwa nchi zinazoshutumiwa ni Ufaransa na licha ya juhudi za hapa na pale zinazofanywa kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili.

Naye Waziri wa nchi katika Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Olivier Nduhungirehe amekiri kwamba, uhusiano baina ya ufaransa na Rwanda si mzuri.“Uhusiano baina ya Rwanda na ufaransa haujatengamaa kwani ufaransa bado inawapa hifadhi watu waliotekeleza mauaji ya kimbari na imeshindwa kuwapeleka mahakamani,” alisema.


Hivi karibuni pia balozi wa Rwanda nchini Uingereza aliionyeshea kidole cha lawama serikali ya London kutokana na kutowakamata washukiwa watano wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ambao inasemekana wamekuwa wakiishi katikka nchi hiyo ya bara Ulaya.

Alipofungua juma la maombolezo wiki iliyopita, Rais Paul Kagame wa nchi hiyo alisema kwamba, licha ya kupita miaka mingi baada ya mauaji hayo, haimaanishi maovu yaliyofanywa dhidi ya Watutsi, yamesahaulika.

Kombora lililoilenga na kuitungua ndege ya Rais wa wakati huo wa Rwanda Juvenal Habyarimana jirani na uwanja wa ndege wa Kigali ndilo lililosababisha kutokea mauaji ya siku 100 dhidi ya Watutsi.

No comments