Update:

Arsenal yalazimishwa sare, Marseille yaibuka kidedea….Siku moja baada ya nusu fainali za kwanza za UEFA Champions League kuchezwa, usiku wa kuamkia leo ilikuwa ni zamu ya kushuhudia nusu fainali za UEFA Europa League, Arsenal wakiikaribisha Atletico Madrid katika uwanja wa Emirates wakati Olympique Marseille walikuwa wenyeji wa FC Salzburg.

Arsenal wameshindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani na kujikuta wakilazimishwa sare ya goli 1-1, kwa matokeo hayo, Arsenal watalazimika kupata ushindi au sare katika mechi ya marudiano itakayopigwa katika uwanja wa Vincente Calderon.

Upande wa Marseille wao wamefanikiwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya FC Salzburg.