Update:

Watu 6 wafariki kufuatia maporomoko ya ardhi yanliosababishwa na mvua kali Kaskazini mwa Nigeria

Watu 6 waripotiwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika maporomoko ya ardhi yaliotokea Kaskazini mwa Nigeria. Maporomoko hayo yametokea baada ya mvua kali kunyesha  katika eneo hilo.  
Kulingana na taarifa zilizotolewa na  shirika la habari la Nigeria la NAN, mvua zilizonyesha  Sokoto ndizo zilizobabisha maporomoko hayo. Majumba kadhaa pia yameporomoka kutokana na mvua hizo.

No comments