Update:

Wasiwasi watanda Zimbabwe baada ya Mugabe kuonekana kuunga mkono mpinzaniWasiwasi umetanda katika chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF, baada ya rais wa zamani Robert Mugabe kuonekana hadharani akiwa ameandamana na jenerali mstaafu ambaye yuko katika kambi ya upizani na ambaye anapanga kuwania urais baadaye mwaka huu.

Mugabe alionekana mwenye tabasamu akiwa amesimama pamoja na Ambrose Mutinhiri, kiongozi cha chama cha upinzani cha National Patriotic Front (NPF) ambacho kinatumai kuindoa madarakani serikali ya hivi sasa katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Hatua ya Mutinhiri ya kujiuzulu ghafla wiki iliyopita kutoka ZANU-PF ilifuatiwa na tangazo lake ambalo liliwashangaza wengi kwamba atakuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha NPF jambo ambalo linaashiria mgawanyiko mkubwa katika chama tawala.

Baada ya picha hiyo ya Mugabe kuenea, vijana wa ZANU-PF wameshiriki katika maandamano ambapo walitoa nara za 'Mauti kwa Mugabe' katika tukio nadra la kubainisha hasira dhidi ya rais huyo wa zamani aliyeiongoza Zimbabwe kwa miongo minne kabla ya kuondolewa madarakani kwa nguvu mwezi Novemba mwaka jana.Rais Mnangagwa wa Zimbabwe

Hayo yanajiri katika hali ambayo duru za karibu na rais wa zamani wa Zimbabwe zimeripoti kuwa Mugabe ana uchungu wa kuondolewa kwenye kiti cha urais alichokalia kwa miaka 37 na hivyo ametangaza uungaji mkono wake kwa chama kipya cha New Patriotic Front .

Mnamo mwezi Januari mwaka huu rais Emmerson Mnangagwa alitangaza kuwa uchaguzi ujao wa Rais, Bunge na serikali za mitaa nchini Zimbabwe utafanyika katika mazingira huru na ya haki.