Update:

Wallace Karia (TFF)" hakuna mchezaji ataruhusiwa kucheza bila kuwa na bima"


Kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacoma (VPL), hakuna mchezaji ataruhusiwa kucheza bila kuwa na bima.

Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia jana wakati wa ufunguzi wa semina ya utawala bora kwa klabu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la semina hiyo ni kutoa elimu kwa viongozi wa vilabu ili kuweza kujiongoza na kutafuta wadhamini.