Update:

Wachambuzi wazungumza zikiwa zimebaki siku chache kulekea pambano la Anthony Joshua na Joseph ParkerWataalamu wa masuala ya masumbwi wanasema tangu Anthony Joshua wa Uingereza aanze kushiriki hili ndio litakuwa pambano lake gumu zaidi kuwahi kupigana kwa kuwa atalazimika kuweka rehani mikanda yake pale atakapomkabili Joseph Parker wa New Zealand.

Pambano hili ni muhimu kwa pande zote mbili kutokana na ukubwa wake japo Joshua amesema ndoto yake kubwa ni kuwa na mikanda mitatu ya WBA, IBF na WBC na kufikia rekodi ya Lewis Lennox ya mwaka 2000.

Katika hatua nyingine wataalamu hao wamesifu uwezo wa Bondia Parker ambaye katika mapambano 24 aliyopigana ameshinda yote huku 18 kati ya hayo akishinda kwa knockout.

Pambano hilo linatarajiwa kupigwa siku ya jumamosi katika ukumbi wa ndani wa uwanja wa Principality mjini Cardiff.