Update:

UTAJIRI WA TRUMP WAPUNGUA KWA DOLA MIL 500Rais wa Marekani, Donald Trump.

UTAJIRI wa Rais wa Marekani, Donald Trump, umeporomoka mwaka huu baada ya kupungua kwa Dola milioni 500 ambazo ni sawa na trioni Sh. 1,126,925,000,000 za Tanzania.Matokeo yake, Trump, mwenye umri wa miaka 71, ameondoka katika nafasi ya 544 ya watu matajiri zaidi duniani, kwa mujibu wa jarida la Forbes, na kuwa mtu wa 766, ambapo hivi sasa ana utajiri wa Dola bilioni 4.

Wakati huohuo, katika orodha hiyo, Jeff Bezos anayemiliki kampuni la Amazon, ndiye tajiri mkubwa zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola bilioni 160, na amempita Bill Gates ambaye ameipoteza nafasi hiyo kwa mara ya sita tangu mwaka 1995.

Habari hiyo mbaya kwa Trump inafuatia pia kupoteza Dola milioni 762, kwa mujibu wa orodha ya Forbes ya mwaka 2017, kutokana na kupungua kwa mali zake mbalimbali kwa maamuzi ya mahakama na idadi ndogo ya wageni waliokuwa wanafikia katika vituo vyake mbalimbali vya michezo ya golf.

Jarida hilo lllilelezea kuporomoka huko kutokana na kupungua kwa thamani za mali zake zilizoko eneo la Manhattan, jijini New York, ambako ndiko kwenye utajiri wake mkubwa zaidi wa majengo.

Utajiri wa kiongozi huyo wa Marekani unatokana na mali aliyokuwa nayo baba yake, Fred, ambao aliuendeleza kabla ya kuwa rais wa kwanza bilionea wa Marekani mnamo Januari 2017. Watoto wake wawili wakubwa zaidi wa kiume, Donald Jr na Eric, ndiyo wanaendesha biashara zake wakati akiongoza taifa hilo.

Hata hivyo, bado kuna wingu la sintofahamu iwapo Trump ni tajiri kama anavyodai ama la.